Video link: Maamuzi sahihi ya kifedha
PROPER FINANCIAL DECISIONS (MAAMUZI SAHIHI YA KIFEDHA)
1. Do I have any doubts in my mind?
Consider yourself first before deciding to do an economic activity or project. Get answers to all important issues before making decisions.
2. Will it contribute to my spiritual growth or hinder me?
Make sure the activity you do does not distract you from your relationship with God. A blessed job does not interfere with your time to worship God, who gives you the strength to work.
3. Will it make me a slave to debt?
If the activity makes you a slave to debt, you will not enjoy it. You will always be stressed, even if you appear rich on the outside. Borrow to maintain a growing business, and not to start a business.
4. Does it contribute to helping the underprivileged and needy?
Don't forget that God did not put you on earth for yourself. You will enjoy life if you touch the life of someone living in a vulnerable environment in your community. We do not help people just because we are rich, but because we know we are on earth for God's purpose.
5. Is it my want (desire) or my need?
Make sure what you are doing is what you need and not what you want. A want is something you desire just because you saw other people possess it. It is not a need that you have discovered for yourself.
MAAMUZI SAHIHI YA KIFEDHA
1. Napata mashaka yoyote katika akili yangu?
Jiridhishe kwanza ndipo uamue kufanya shughuli au mradi wa kiuchumi. Pata majibu ya masuala yote muhimu kabla ya kufanya maamuzi.
2. Yatachangia katika ukuaji wangu wa kiroho au yatanizuia?
Hakikisha shughuli inayofanya haikutoi katika uhusiano wako na Mungu. Kazi yenye baraka ni ile ambayo haivurugi muda wako wa kumuabudu Mungu anayekupa nguvu za kufanya kazi.
3. Yatanifanya niwe mtumwa wa madeni?
Kama shughuli hiyo itakufanya kuwa mtumwa wa madeni, hutaifurahia. Muda wote utakuwa na msongo wa mawazo hata kama kwa nje unaonekana kwamba u tajiri. Kopa kwa ajili ya kuendeleza biashara inayokua na sio kwa ajili ya kuanzisha biashara.
4. Yanachangia katika kusaidia wasiojiweza na wahitaji?
Usisahau kwamba Mungu hakukuleta duniani kwa ajili yako mwenyewe. Utafurahia maisha kama unagusa maisha ya mtu fulani anayeishi mazingira hatarishi katika jamii yako. Hatusaidii watu kwa vile tu matajiri bali kwa vile tunajua tuko duniani kwa kusudi la Mungu.
5. Ni matamanio yangu au ni hitaji langu?
Hakikisha jambo unalofanya ni hitaji lako na sio tamanio lako. Tamanio (want) ni kitu ambacho unataka ukipate kwa vile tu umeona watu wengine wanacho. Sio hitaji (need) ambalo umeligundua wewe mwenyewe.
Dr. Lawi Mshana, Freelance Facilitator, +255 712924234, Tanzania
0 Comments
Karibu sana na ujisikie huru kushirikisha mawazo yako au kuuliza swali tujifunze pamoja (Welcome and feel free to share your thoughts or ask questions so we can learn together)