Video link: Mambo muhimu katika mafanikio ya maisha
KEYS TO SUCCESS IN LIFE (MAMBO MUHIMU KATIKA MAFANIKIO YA MAISHA)
1. Identify your passions and your definition of success— If you are passionate about doing something, will not get bored quickly. But loving what you do is not enough. You also need to identify your definition of success. Your definition of success could be changing yourself, touching the lives of others, or showing yourself to others.
2. List your goals and what you can do to achieve them – Some people have no goals. Others have goals but do not see their ability to achieve them. So they wait for someone to help them achieve them. As a result, they are late. They forget that they are a great resource.
3. Ask yourself if what you are doing is helping you get where you want to go – Having goals alone is not enough. We also need to do things that help in achieving those goals. We must have a purpose and protect ourselves from being sidetracked.
4. Manage your money even if it is small – To know the value of a small amount of money, go buy something worth one thousand shillings when you have nine hundred shillings. You will see that you are stuck because you lack one hundred shillings. Find out what your major expenses are for and strive to reduce those expenses. But also find out your net pay or profit so that you do not console yourself that you have a lot of money whereas you are eating up capital.
5. Manage your time – Make sure to use your time wisely. Know the order of the tasks you will do tomorrow. Also, do not forget to have a deadline to complete your tasks. If you do not have a deadline, you will be procrastinating without seeing the consequences.
MAMBO MUHIMU KATIKA MAFANIKIO YA MAISHA
1. Tambua shauku zako na tafsiri yako ya mafanikio – Mambo ambayo una shauku ya kuyafanya hutaweza kuchoka haraka. Lakini kupenda unachofanya hakutoshi. Unatakiwa pia kutambua tafsiri yako ya mafanikio ni ipi. Tafsiri yako ya mafanikio inaweza kuwa kubadilika wewe mwenyewe, kugusa maisha ya wengine, au kujionyesha kwa wengine.
2. Orodhesha malengo yako na unachoweza kufanya katika kuyatimiza – Kuna watu hawana malengo yoyote. Lakini pia wapo wenye malengo lakini hawaoni uwezo wao katika kutimiza baadhi ya malengo. Hivyo wanasubiri mtu fulani awasaidie kuyatimiza. Matokeo yake wanachelewa. Wanasahau kwamba wao wenyewe ni raslimali kubwa.
3. Jiulize kama unachofanya kinakusaidia kufika unapotaka kwenda – Kuwa na malengo peke yake hakutoshi. Tunatakiwa pia tufanye mambo ambayo yanasaidia katika kutimiza malengo hayo. Lazima tuwe na kusudi na kujilinda tusitoke nje ya mstari.
4. Simamia pesa zako hata kama ni kidogo – Ili ujue hata pesa ndogo ina thamani, nenda kununua kitu cha shilingi elfu moja ukiwa na shilingi mia tisa. Utaona ukikwama kwa sababu tu ya kukosa shilingi mia moja. Gundua matumizi yako makubwa ni ya kitu gani na kujitahidi kupunguza matumiza hayo. Lakini pia gundua kipato chako halisi au faida (net pay/profit) ili usijifariji kwamba unashika pesa nyingi na kumbe unakula mtaji.
5. Simamia muda wako – Jali kutumia vizuri muda wako. Fahamu kazi utakazofanya kesho na kwamba utaanza na kazi ipi na kumaliza na ipi. Usisahau pia kuwa na muda wa mwisho wa kumaliza kazi zako (deadline). Ukiwa huna muda wa mwisho utakuwa unaahirisha bila kuona madhara ya kufanya hivyo.
Dr. Lawi Mshana, Freelance Facilitator, 0712-924234, Korogwe, Tanga, Tanzania
0 Comments
Karibu sana na ujisikie huru kushirikisha mawazo yako au kuuliza swali tujifunze pamoja (Welcome and feel free to share your thoughts or ask questions so we can learn together)