Video: KIPINDI MAALUM CHA KLINIKI YA UPONYAJI
KIPINDI MAALUM CHA KLINIKI YA UPONYAJI (APOSTOLIC
HOUR)
Kliniki ya uponyaji ni kipindi nje ya muda wa ibada ambacho ni maalum kwa ajili ya watu wenye matatizo yasiyosikia dawa.
Mtu anapohitaji huduma hii anapaswa kufanyiwa mahojiano ya
uchunguzi (diagnosis) na awe tayari kushiriki vipindi kadhaa mpaka atakapokuwa
huru kwelikweli. Kuna wakati Mungu haponyi kwa MUUJIZA wa papo kwa papo bali
anaponya kwa MCHAKATO. Mtu anapoombewa anashauriwa na kuelezea mabadiliko
anayoyaona mpaka atakapofunguliwa.
Mk 8:22-26 “22 Wakafika Bethsaida, wakamletea kipofu, wakamsihi amguse. 23 Akamshika mkono yule kipofu, akamchukua nje ya kijiji, akamtemea mate ya macho, akamwekea mikono yake, akamwuliza, Waona kitu? 24 Akatazama juu, akasema, Naona watu kama miti, inakwenda. 25 Ndipo akaweka tena mikono yake juu ya macho yake, naye akatazama sana; akawa mzima, akaona vyote waziwazi. 26 Akampeleka nyumbani kwake, akisema, Hata kijijini usiingie.”
Hata hivyo lazima mhitaji (mteja) apangiwe muda maalum (appointment) kwa vile ni huduma inayohitaji kuombea kwa ufuatiliaji wa karibu na sio kuombea kundi la watu kwa pamoja. Kundi linaombewa muda wa ibada.
Huduma hii inatolewa bure na hatutoi wala kuuza vifaa vyovyote kwa vile hatujawahi kugharamia karama tulizopewa na Bwana. Mathayo 10:8 “Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.”
Kuna wakati huduma hii inafanyika kwa njia ya mtandao.
Dr.
Lawi Mshana, Korogwe, Tanga, Tanzania
0 Comments
Karibu sana na ujisikie huru kushirikisha mawazo yako au kuuliza swali tujifunze pamoja (Welcome and feel free to share your thoughts or ask questions so we can learn together)