Ticker

6/recent/ticker-posts

Basic Math Practice Free (Mazoezi ya Hisabati Bila Malipo) - Join our team please



Video: Basic Math Practice Free
 

Basic Math Practice Free (Mazoezi ya Hisabati Bila Malipo)

ASILIMIA 25 pekee ya wanafunzi waliofanya mtihani wa somo la hisabati, Mtihani wa Taifa Kidato cha Nne Mwaka 2024 nchini, walifaulu mtihani huo, huku asilimia 74.6 wakifeli. Matokeo ya ufaulu wa Hisabati kidato cha nne mwaka 2024

Kupitia Tovuti hii ya kujengea uwezo jamii, tunaanza kufanya mazoezi ya Hisabati (past papers) bure kwa ajili ya wanafunzi wa sekondari (O-level). Tunaunga mkono juhudi za serikali na walimu katika kuwatia moyo wanafunzi wapende, wasome na kufaulu somo hili. Tutatoa maelezo kwa kuchanganya Kingereza na Kiswahili ili kurahisisha uelewa wa mwanafunzi.

Mpango huu ni wa kuwashirikisha wanafunzi wa zamani ambao tulipenda na kufaulu somo la Hisabati bila kujali kwa sasa tunafanya kazi gani. Unaweza kuniandikia nikupatie maswali ya Topic ambazo ni nzuri zaidi kwako.

Unaweza kutuma video kwangu ukiwa una-solve swali ili mradi katika video hiyo utamke kwamba unaruhusu Lawi Mshana a-edit na ku-publish kwa ajili ya wanafunzi kujifunza na ku-download bure. Pia utataja kwamba unaitwa nani, kutoka wapi, simu yako na unafanya kazi gani. Lengo kuu la kuedit ni kuongeza sauti kama ilikuwa chini na kupunguza ukubwa wa file.

Mzazi au mlezi wa mwanafunzi akiona analetewa ujumbe wa kuchagua anuani ya baruapepe ya Gmail anaweza kulazimika kufungua anuani ili iwe rahisi kuziona video na kudownload bure. Kufungua anuani ya Gmail ni bure.

Jinsi ya kupata sehemu mazoezi ya Hisabati yalipo kwenye hii Tovuti:

Uta-scroll upite makala zote na sehemu yenye kichwa cha MITANDAO YA JAMII. Baada ya hapo utaona PAGES (KURASA) ambapo chini yake utaona kiungo (link) cha BASIC MATH PRACTICE FREE.

Ukibofya utaletewa SELECT AN ACCOUNT (CHAGUA AKAUNTI). Kama huna anuani ya barua pepe fungua anuani kwa vile ni huduma ya bure. Unatakiwa ufanye hivyo kwa vile Google ndio wamenisaidia kuhifadhi video hizo bure.  Huna sababu ya kuona ni usumbufu kwa vile unapatiwa huduma hii bila malipo.

Njia nyingine ya kuingia kwenye sehemu hiyo ni kwa ku-download na ku-install App yangu ya ‘Faith Empower’ na kubofya sehemu ya Tovuti. Unaweza kuipata App hiyo hapahapa kwenye Tovuti sehemu iliyoandikwa DOWNLOAD APP.

Karibu sana turudishe shukrani yetu kwa jamii ambayo imetupa malezi mazuri.

Dhima ya Beyond Four Walls ni kujengea uwezo jamii ishinde changamoto kwa kutumia mbinu shirikishi za maendeleo. 

Dr. Lawi Mshana, 0712924234, Korogwe, Tanga, Tanzania

Post a Comment

0 Comments