Ticker

6/recent/ticker-posts

3. Relate well with people because they have your blessings. (Jali watu maana wana baraka zako)


 Video:Na 3 Jali watu maana wana baraka zako

3. Relate well with people because they have your blessings.

(Jali watu maana wana baraka zako)

Become best friends with God. Pro 3:3,4 “Let not mercy and truth forsake you; Bind them around your neck, Write them on the tablet of your heart, And so find favor and high esteem In the sight of God and man.” If you want a blessed friendship with God, be honest and be a person who cares about people. Maintain a good relationship with God at all times. Some people care about the relationship with God only during worship. When they are at home or work they behave very strangely. They oppress people and torture them. Wherever you go, your life should be the same. You have no reason to change your living standards because you are with strangers. If you care about people, you will get wisdom and understanding. God gave Oholiab and Bezalel the skills to design and make things for the temple. Ex 36:1 “"And Bezalel and Aholiab, and every gifted artisan in whom the LORD has put wisdom and understanding, to know how to do all manner of work for the service of the sanctuary, shall do according to all that the LORD has commanded."” Even you, God can give you favor before God and before men. If God gives you favor, people will care about you, listen to you, and remember you because God uses people to bless you. Therefore, you cannot be on good terms with God without caring about people and expect to prosper. The cross has two parts - vertical and horizontal. This indicates that we should not only have a relationship with God but also with people.

Unatakiwa kuwa rafiki wa Mungu. Mit 3:3,4 “Rehema na kweli zisifarakane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako. Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu.” Ukitaka urafiki na Mungu wenye baraka uwe mkweli na uwe mtu anayejali watu. Jali kuwa na uhusiano mzuri na Mungu wakati wote. Watu wengine wanajali uhusiano na Mungu wakati wa ibada tu. Wanapokuwa nyumbani au kazini wana tabia za ajabu sana. Wanaonea watu na kuwatesa. Kila mahali unapokwenda Maisha yako yawe kiwango kilekile. Huna sababu ya kubadilisha viwango vya kuishi kwako kwa sababu uko na watu wasiokujua. Ukijali watu utapata kibali na akili nzuri. Kuna watu walipewa na Mungu akili za kubuni na kutengeneza vitu vya hekalu. Kutoka 36:1 “Basi Bezaleli na Oholiabu watatenda kazi, na kila mtu mwenye moyo wa hekima, ambaye Bwana amemtia akili na hekima ili ajue kufanya kazi hiyo yote kwa huo utumishi wa mahali patakatifu, kama hayo yote Bwana aliyoyaagiza.” Hata wewe Mungu anaweza kukupa kibali mbele za Mungu na mbele za wanadamu. Mungu akikupa kibali watu watakujali, watakusikiliza na kukukumbuka kwa vile Mungu anatumia watu kukubariki. Kwa hiyo huwezi kuwa na tabia nzuri kwa Mungu tu bila kujali watu halafu ufanikiwe. Msalaba una sehemu mbili – wima na ulalo. Hii inamaanisha kwamba hatutakiwi kuwa na uhusiano na Mungu peke yake bali pia tuwe na uhusiano na watu.

Bofya video usikilize ujumbe huu utaelewa zaidi.

Dr. Lawi Mshana, Freelance Facilitator & Public Speaker, +255712924234, Tanzania

Post a Comment

0 Comments