Ticker

6/recent/ticker-posts

WELCOME TO JOIN OUR EFFORTS FOR THE COMMUNITY (KARIBU UUNGE MKONO JUHUDI ZETU KWA AJILI YA JAMII)





WELCOME TO JOIN OUR EFFORTS FOR THE COMMUNITY 

(KARIBU UUNGE MKONO JUHUDI ZETU KWA AJILI YA JAMII)

We are thankful for successfully holding our Beyond Four Walls annual meeting where the guest of honor was the Acting Town Community Development Officer and Assistant Registrar of NGOs, Mr. Fredrick Kitundu. The guest of honor emphasized the importance of continuing to care for and protect children from harm and fulfill all legal requirements of the NGO, including paying annual fees and sending implementation reports on time.

Since children aged 10-17 are our main target, we want to ensure they participate in our meetings, become advocates of their issues, and get equipped for later leadership. We often ignore children at the family level. We don't involve them in decision-making in family meetings. As a result, the implementation becomes difficult because they have unanswered questions and sometimes feel like they are being bullied even though the decision-makers have good intentions. Participation and involvement help people value decisions and see themselves as owning the vision.

We have various plans that will be successful if we collaborate well with the local government, other organizations, religious institutions, companies, individuals, and other development partners.

We believe that all citizens can contribute to the development instead of being overdependent on foreign aid which sometimes robs us of our dignity and deprives us of our freedom.

A certain stakeholder bought a plot for us to build a small office with a small hall (sub-office) in Ihumwa, Dodoma. (see the photo)

Probably after building your house, you have leftover building materials or any used items. Let us know, please.

Our mission is to build the capacity of the community to overcome vulnerability, poverty, and dependency through participatory development.

Contact us if you are inspired to donate anything, be it money or building materials, furniture, computers, clothes, canvases, vehicles, etc.

May God grant you a year full of grace.

           KARIBU UUNGE MKONO JUHUDI ZETU KWA AJILI YA JAMII

Tunashukuru kwa kufanikiwa kufanya mkutano wetu wa mwaka wa Beyond Four Walls ambapo mgeni rasmi alikuwa Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Mji na Msajili Msaidizi wa NGOs, Ndugu Fredrick Kitundu. Mgeni rasmi alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuwajali na kuwalinda watoto dhidi ya uhatarishi na kutimiza matakwa yote ya kisheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) ikiwa ni pamoja na kulipa ada za mwaka na kutuma ripoti za utekelezaji kwa wakati.

Kwa vile watoto wa miaka 10-17 ni walengwa wetu wakuu, tunapenda kuhakikisha wanashiriki mikutano yetu, wanahusika katika maamuzi yanayowahusu na kuandaliwa kwa ajili ya uongozi siku za usoni. Mara nyingi katika ngazi ya familia tumezoea kuwapuuza watoto. Hatuwahusishi katika maamuzi kwenye vikao vya familia. Matokeo yake, utekelezaji unakuwa mgumu kwa vile wana maswali yasiyo na majibu na wakati mwingine wanaona kama wanaonewa kumbe wafanya-maamuzi wana makusudi mazuri mazuri kwa ajili yao. Ushiriki na ushirikishwaji unasaidia watu kuthamini maamuzi na kujiona wanayamiliki maono.

Tuna mipango mbalimbali ambayo itafanikiwa kama tutashirikiana vizuri na serikali za mitaa, mashirika mengine, taasisi za dini, makampuni, watu binafsi na wadau wengine wa maendeleo.

Tunaamini kwamba raia wote tunaweza kuchangia maendeleo yetu badala ya kuwa tegemezi wa misaada kutoka nje ambayo wakati mwingine inatunyang’anya utu wetu na kutunyima uhuru.

Kuna mdau alitununulia kiwanja kwa ajili ya kujenga ofisi ndogo yenye ukumbi mdogo (sub-office) Ihumwa, Dodoma. (tazama picha)

Pengine baada ya kujenga nyumba yako umebakiwa na vifaa vya ujenzi au una vitu usivyovitumia kwa sasa. Tujulishe tafadhali.

Dhima yetu ni kujengea uwezo jamii ishinde uhatarishi, umaskini na utegemezi kwa kutumia njia shirikishi za maendeleo.

Wasiliana nasi kama umeguswa kuchangia kiasi chochote cha fedha au vifaa kv vifaa vya ujenzi, fanicha, kompyuta, nguo, maturubai, vyombo vya usafiri nk

Mungu akupe mwaka wenye neema tele.

Beyond Four Walls (NGO), +255712924234, Korogwe, Tanga, Tanzania.

 

Post a Comment

0 Comments