Tunapenda
kutoa shukrani za dhati kwa wote mlioguswa kujitolea kushirikiana nasi katika
huduma za mwaka 2025. Mpo ambao mmeahidi kuchangia sadaka ya upendo ili
kutegemeza huduma tunazotoa kwa jamii kila mwezi. Lakini pia mpo mlioahidi
kuchangia raslimali zingine kulingana na upatikanaji wenu kv muda wenu, ujuzi wenu,
uzoefu wenu nk. Tumetiwa moyo kuona kwamba ingawa baadhi yenu tumefahamiana mtandaoni
tu mmetambua uzito wa huduma hii ambayo inawafikia watu bure bila kuwatoza
chochote. Hamkujali umbali wala tofauti za kidini. Mungu mwenyewe atawalipa kwa
moyo huo wa utoaji.
Tunaamini
kwamba kanzi data (database) ya taarifa zenu itatusaidia pamoja na wadau
wengine wa maendeleo watakaohitaji valantia (volunteers) kwa ajili ya huduma za
jamii.
Tumepata
valantia kwa ajili ya huduma zifuatazo:
1. Kufundisha masomo ya kisayansi mfano hisabati,
kufundisha kompyuta kwa vijana na jamii inayowazunguka 2. Kutoa ushauri wa kiuandishi wa tafiti mbalimbali na
kusaidia kuchakata data ili kuzitolea ufumbuzi wa kisayansi 3. Kuchapisha maudhui yanayohusiana na tafiti
mbalimbali za afya, mazingira na elimu ili kufikia malengo ya taifa 4. Kukusanya taarifa kwenye miradi ya kijamii (data
collection) 5. Kuwezesha mijadala, midahalo na mafunzo ya vijana
katika jamii 6. Kujengea uwezo jamii katika
usimamizi bora wa mikopo 7. Video (video directing and graphic
design) 8. Kufundisha watoto wenye ulemavu 9. Kutafsiri vitabu na kukalimani
semina na mikutano 10. Kutafsiri na kukalimani lugha ya
alama 11. Utunzi na uandishi wa nyimbo 12. Kuandaa matukio (event
coordinating) 13. Ushauri wa kujengea uwezo kibinafsi
(mentoring and coaching) 14. Kuhamasisha michango kwa ajili ya
huduma za jamii (fundraising) 15. Shughuli za kihasibu na fedha
(accountancy and finance) 16. Uandishi wa makala mbalimbali
(content writing) 17. Kuwezesha kuhusu ujuzi wa kufanya
biashara kidijitali 18. Kuwezesha jamii ijue kuhusu afya ya akili nk Tunaendelea kutoa wito kwa jamii ituunge mkono ili tuweze kuwafikia wengi zaidi hasa hasa wale wanaoishi pembezoni na katika mazingira hatarishi bila ubaguzi wa kidini, kikabila na kimatabaka. Mungu anapenda sana kuona watu wake wanatoa sadaka kwa moyo wa kupenda bila kulazimishwa. Kutoka 35:29 “Wana wa Israeli wakaleta sadaka za kumpa Bwana kwa moyo wa kupenda; wote, waume kwa wake, ambao mioyo yao iliwafanya kuwa wapenda kuleta kwa hiyo kazi, ambayo Bwana aliamuru ifanywe kwa mkono wa Musa.” 2
Wakorintho 9:7 “Kila mtu na atende
kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana
Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.” Mdo 20:35 “Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa
kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya
Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.” Tunakutakia mwaka mpya wenye fursa nyingi ili uzidi kuwa baraka kwa wengine. Karibu sana katika ofisi zetu za kujenga uwezo wa kushinda umasikini, utegemezi na uhatarishi bila malipo yoyote. Unaweza kuwa na uwezo na elimu lakini huoni fursa zilizoko mbele yako. Beyond Four Walls (NGO),
+255712924234, Korogwe, Tanga, Tanzania |
0 Comments
Karibu sana na ujisikie huru kushirikisha mawazo yako au kuuliza swali tujifunze pamoja (Welcome and feel free to share your thoughts or ask questions so we can learn together)