OMBI KWA WATETEZI WA HAKI ZA WATOTO
Kuna msamaria amemsaidia msichana akasoma hadi kumaliza
darasa la saba na kisha akamrudisha kwa mzazi wake anayeishi mkoa wa mbali sana
na Korogwe. Msichana huyo amefaulu na kupangwa shule ya sekondari ya hapa
Korogwe mjini. Mzazi wa msichana huyo anaishi katika mazingira magumu sana
kiasi kwamba anasema hata akisaidiwa kusomeshewa mtoto, hawezi hata
kumsafirisha arudi Korogwe mjini. Kwa maneno mengine ni sawa na kusema huo ni
mwisho wa elimu wa msichana huyu.
Naomba yeyote anayeweza kuhusika kwa namna yoyote ili tumsaidie
msichana huyu asome, awasiliane na sisi.
Mungu hajatuita kuombea na kufundisha peke yake. Ametuita
pia KUWASAIDIA WANAOONEWA, KUWAPATIA WANYONGE HAKI ZAO NA KUWATETEA WAJANE. Isaya
1:17 “jifunzeni kutenda mema; takeni
hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni
mjane.”
Mungu akubariki sana kwa kuguswa na hitaji la kutimiza ndoto
za msichana huyu.
Beyond Four Walls, 0712924234, Korogwe, Tanga, Tanzania
Dhima ya Beyond Four Walls ni kujengea uwezo jamii ishinde
umasikini, utegemezi na uhatarishi kwa kutumia mbinu shirikishi.
0 Comments
Karibu sana na ujisikie huru kushirikisha mawazo yako au kuuliza swali tujifunze pamoja (Welcome and feel free to share your thoughts or ask questions so we can learn together)