Video: Na 15: Unahitaji muda wa kutosha kutambua tabia halisi ya mtu
Maisha bora Na 15: Unahitaji muda wa kutosha kutambua tabia halisi ya mtu
Kanisa haliwezi kuwa imara kama familia sio imara. Muda unaotosha kutengeneza tabia ya mtu ni nyumbani kwenye familia kuliko kanisani. Nyumbani ndipo mtu anakuwa katika tabia yake halisi. Mungu alianzisha Familia kabla ya Kanisa. Kimsingi, mpango wa kuanzisha Kanisa ulikuja baada ya anguko la familia ya kwanza. Lengo la Kanisa ni kuwarudisha au kuwarejeza wanadamu kwenye msingi. Maana ya Kanisa kwa Kiyunani ni “ek klesia” yaani “walioitwa baada ya kupotea” (called out ones). Kwa hiyo kama mwanadamu hangepotea, Kanisa halingekuwepo. Mungu angefanya kazi na Familia. Familia ilianzishwa na Adamu wa kwanza na Kanisa likaanzishwa na Adamu wa mwisho (Yesu Kristo). 1 Wakorintho 15:45 “Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha.”
Bofya usikilize ujumbe huu utaelewa zaidi.
Dr. Lawi Mshana, Freelance Facilitator
& Public Speaker, +255712924234, Tanzania
0 Comments
Karibu sana na ujisikie huru kushirikisha mawazo yako au kuuliza swali tujifunze pamoja (Welcome and feel free to share your thoughts or ask questions so we can learn together)