Video: Na 13: Kwanini shetani analenga zaidi kuwatumia wanawake?
Maisha bora Na 13: Kwanini shetani analenga zaidi kuwatumia wanawake?
Mwa 2:18 “Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.” Neno msaidizi katika andiko hili lina maana ya kuokoa maisha ya mwanaume. Mwanamke alipewa uwezo wa ulinzi katika ndoa. Yeremia 31:22 “…Kwa maana Bwana ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume.” Kwa vile shetani anajua uwezo na jukumu alilopewa mwanamke, amekuwa akilenga kumtumia zaidi ili iwe rahisi kumpata mwanaume. Mwanamke aliumbwa kwa ubavu wa Adamu na sio kwa udongo moja kwa moja kama ilivyokuwa kwa Adamu. Mungu alichomoa ubavu kwa Adamu ili ahisi kupungukiwa na kuona umuhimu wa mwanamke katika maisha yake.
Bofya usikilize ujumbe huu utaelewa zaidi.
Dr. Lawi Mshana, Freelance Facilitator & Public Speaker, +255712924234, Tanzania
0 Comments
Karibu sana na ujisikie huru kushirikisha mawazo yako au kuuliza swali tujifunze pamoja (Welcome and feel free to share your thoughts or ask questions so we can learn together)