Ticker

6/recent/ticker-posts

Maisha bora Na 7: Unajua Mungu alimaanisha nini aliposema wanandoa waambatane?


 Video: Na 7: Unajua Mungu alimaanisha nini aliposema wanandoa waambatane?

Maisha bora Na 7: Unajua Mungu alimaanisha nini aliposema wanandoa waambatane?

Tunaposoma Mwa 2:24 “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja,” tunaona kwamba jambo la pili muhimu kwa wanandoa ni ‘kuambatana’ – kushirikishana mipango yenu na siri zenu. Msiwe na siri na watu wengine nje ya ndoa yenu. Mfanye mambo yanayowaleta pamoja na kutengeneza mazingira yanayowezekana ya kuwafanya muwe karibu, mtembee pamoja. Haina maana kwamba kila mahali muende pamoja lakini mjitahidi kuwa karibu kadiri inavyowezekana. Mtu akiwa mbali kwa kipindi kirefu ni rahisi mwenzake kutomuwazia tena (out of sight, out of mind).

Shetani anapata nafasi wanandoa wanaposhindwa kushirikishana na kuaminiana. Waefeso 4:27 “wala msimpe Ibilisi nafasi.”

Sikiliza kisa kilichotokea kwa wanandoa wasioaminiana.

Dr. Lawi Mshana, Freelance Facilitator & Public Speaker, +255712924234, Tanzania

Post a Comment

0 Comments