Video: Na 6: Unajua hatari ya kuandaa harusi badala ya ndoa na maisha?
Maisha bora Na 6: Unajua hatari ya kuandaa harusi badala ya
ndoa na maisha?
Vijana wasiandae harusi kubwa na kusahau kuandaa maisha. Kuandaa harusi kunasababisha ukomo wa mawazo ya kijana kuwe siku ya harusi. Matokeo yake hawa wanandoa wapya wanakuwa na madeni makubwa baada ya harusi kiasi cha kuuza zawadi ili kulipa madeni.
Wazazi tuwaandae vijana wajitegemee baada ya kuoa. Wasije mara kwa mara nyumbani wakilia shida ya chakula. Kijana naye akishaoa asimlinganishe mke wake na mama yake mzazi. Mke ni mwanamke tofauti kabisa ambaye Mungu amempa hivyo amuombe Mungu amuwezeshe kufahamu amepewa mke wa namna gani. Mhubiri 9:9 “Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye, siku zote za maisha yako ya ubatili, ulizopewa chini ya jua; siku zote za ubatili wako, kwa maana huo ni sehemu yako ya maisha; na katika taabu zako ulizozitaabika chini ya jua.”
Dr. Lawi Mshana, Freelance Facilitator
& Public Speaker, +255712924234, Tanzania
0 Comments
Karibu sana na ujisikie huru kushirikisha mawazo yako au kuuliza swali tujifunze pamoja (Welcome and feel free to share your thoughts or ask questions so we can learn together)