Ticker

6/recent/ticker-posts

Maisha bora Na 5: Unajua hatari ya kuoa na kukaa na mke kwa wazazi wako?


 Video: Na 5: Unajua hatari ya kuoa na kukaa na mke kwa wazazi wako?

Maisha bora Na 5: Unajua hatari ya kuoa na kukaa na mke kwa wazazi wako?

Mwa 2:24 “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.” Hili andiko limetaja mambo matatu muhimu kwenye ndoa. Kufunga ndoa kanisani peke yake hakutoshi kama mambo hayo hayatazingatiwa. Mambo hayo ni KUACHA (KUONDOKA KWA WAZAZI), KUAMBATANA NA KUWA MWILI MMOJA.

Hatua ya kwanza ni KUACHA (kuondoka kwa wazazi). Ndiyo maana hatutaki mtu akioa akae na mkewe kwa wazazi wake. Ni rahisi kumkosea Mungu kwa vile Mungu ameagiza hivyo. Mungu anataka waanze maisha yao mapya na mfumo wao mpya wa ndoa hata kama maisha yao ni duni. Wazazi wanatakiwa kuwashauri tu na sio kuwalazimisha kufuata mfumo wao wa maisha.

Dr. Lawi Mshana, Freelance Facilitator & Public Speaker, +255712924234, Tanzania

Post a Comment

0 Comments