Ticker

6/recent/ticker-posts

Maisha bora Na 4: Unajua mapungufu yako katika kuomba?


 Video: Na 4: Unajua mapungufu yako katika kuomba?

Maisha bora Na 4: Unajua mapungufu yako katika kuomba?

Tii mara moja Mungu anaposema na wewe kuhusu jambo lolote ndipo utafanikiwa. Mama yake Bwana Yesu alitoa ushauri huu kwenye harusi na walipoufuata bila maswali waliafanikiwa. Yohana 2:5 “Mamaye akawaambia watumishi, Lo lote atakalowaambia, fanyeni.”

Ile tunayoiita sala ya Bwana sio sala hasa bali ni fundisho la Bwana Yesu kuhusu kuomba. Bwana Yesu aliwafundisha wanafunzi wake walipomuomba awafundishe jinsi ya kuomba. Lk 11:1,2 “Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake Akawaambia, Msalipo, semeni, Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.

Sio vizuri kuomba riziki kwa ujumla. Tambua riziki yako ya leo kwa kuitaja ni ipi. Mt 6:11 “Utupe leo riziki yetu.”

Wakati hasa ambapo Bwana Yesu aliomba (Sala ya Bwana) ni katika Yohana 17. “Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako.” (Yn 17:9)

Dr. Lawi Mshana, Freelance Facilitator & Public Speaker, +255712924234, Tanzania

Post a Comment

0 Comments