Mungu alipomuumba mwanadamu kama familia alikusudia tuishi milele duniani bila dhambi tukiwa tunatawala dunia. Mwanzo 1:26 “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.” Mungu alianzisha koloni hapa duniani linalosimamiwa na mwanadamu. Hatukutumwa kuhubiri dini bali kutawala katika ufalme wake. Yohana Mbatizaji alihubiri ufalme wa Mungu na Bwana Yesu pia alihubiri ufalme na sio dini. Hata Bwana Yesu alipoombwa na wanafunzi wake kuwafundisha kuomba aliwaambia waombe kwamba ufalme wa Mungu uje duniani.
Ni kweli tumepewa kazi ya kuhubiri Injili lakini kusudi kubwa ni KUTAWALA. Tunahubiri Injili ili kumrudisha mwanadamu katika kusudi la Mungu na kumrudishia mamlaka yake ili atawale.
Ndiyo maana kuna wakati Mungu atatuonjesha kutawala – tutatawala na Bwana kwa miaka 1000 katika ufalme usio na dhambi yoyote.
Dr. Lawi Mshana, Freelance Facilitator
& Public Speaker, +255712924234, Tanzania
0 Comments
Karibu sana na ujisikie huru kushirikisha mawazo yako au kuuliza swali tujifunze pamoja (Welcome and feel free to share your thoughts or ask questions so we can learn together)