Kuanzia tarehe 21 Julai 2024
nitakuwa jijini Dodoma kwa ajili ya kutoa ushauri wa kujenga uwezo katika masuala
mbalimbali yanayohatarisha maisha.
Mtu anaweza kuwa na uwezo
uliojificha (potential) ndani yake lakini hajui. Lakini pia mtu anaweza kuwa
chanzo cha changamoto zake lakini anahamishia lawama kwa wengine.
Mfano wa masuala ambayo
nitatoa ushauri bila malipo:
1. Wanandoa ambao mnakutana
na changamoto za mahusiano ambazo mmeshindwa kupata ufumbuzi wake (mkiwa wote
wawili ni vizuri zaidi).
2. Una ujuzi lakini unashindwa kutambua na kutumia fursa na
raslimali zilizopo. Wenye ujuzi kama wewe wanafanikiwa lakini wewe unashindwa
uanzie wapi.
3. Jinsi ya kukabiliana na uhatarishi unaokukabili mara
kwa mara katika mazingira yako ya nyumbani, kazini, shuleni na katika jamii.
4. Kutambua sababu za kutopokea mabadiliko au maendeleo ingawa
unamcha na kumtumikia Mungu vizuri.
5. Jinsi ya kufanikiwa kimaisha bila kutawaliwa na madeni
yasiyolipika.
6. Unashindwa kubadili maisha yako hata pale unapopata fedha
au kipato kama wengine.
7. Unashindwa kufanya maamuzi sahihi kuhusu maisha yako (mara
nyingi unajutia mambo unayoyafanya)
8. Umepoteza tumaini la maisha sababu ya hali yako.
Mfano, unaishi na VVU na unajiona kama ni mwisho wa maisha yako.
9. Kuna tabia imekutawa sana ingawa huipendi na huoni
namna yoyote ya kushinda hali hiyo. Nk.
Kumbuka huduma hii inatolewa bure bila malipo yoyote na
mnaweza kushauriwa kibinafsi au kwa kundi kama hitaji linafanana.
Pia ratiba ikiruhusu naweza kuwafikia hapo mlipo kama ni
kikundi. Karibuni sana.
Kwa mawasiliano ili kupanga muda wa kupata huduma hii,
tumia simu hizi: 0712-924234 na 0629-462402
Dr Lawi Mshana
0 Comments
Karibu sana na ujisikie huru kushirikisha mawazo yako au kuuliza swali tujifunze pamoja (Welcome and feel free to share your thoughts or ask questions so we can learn together)