Ticker

6/recent/ticker-posts

TUVUNJE MAAGANO YA SHETANI MASHULENI (WIKI LA MAOMBEZI YA UKOMBOZI KWA WANAFUNZI)

TUVUNJE MAAGANO YA SHETANI MASHULENI (WIKI LA MAOMBEZI YA UKOMBOZI KWA WANAFUNZI) 

TUVUNJE MAAGANO YA SHETANI MASHULENI (WIKI LA MAOMBEZI YA UKOMBOZI KWA WANAFUNZI)

Unajua watoto wetu wanakaa muda mrefu mashuleni kuliko majumbani na katika nyumba za ibada? Unajua baadhi ya mashule yamejengwa katika maeneo ambayo awali yalikusudiwa kuwa ya matumizi mengine? Unajua hata baadhi ya walimu wanaathiriwa na roho ya ‘backwardness and retardation’ katika maisha sababu ya unajisi wa mashuleni? Fuatilia ujumbe huu na kushiriki katika maombi.

Tangazo

Wiki hii (Jtatu hadi Ijumaa) hapa kanisa la TLMC (Hema) Korogwe mjini tutakuwa na maombezi maalum ya UKOMBOZI KWA WANAFUNZI wanaoamini nguvu ya maombi. Wapo wenye changamoto tangu walipopoteza madaftari yao au kutamkiwa kwamba hawana akili. Maombi hayo yataambatana na ufuatiliaji wa maendeleo yao kitaaluma (kwa wale ambao wana changamoto). Tutaombea hata madaftari yao. Wanafunzi wa shule ya msingi watafika asubuhi na wa sekondari jioni lakini kwa KIBALI MAALUM KUTOKA KWA WAZAZI WAO. Hasahasa kwa wale ambao hawana vipindi shuleni wakati huu wa likizo. Kila siku itakuwa na masomo maalum ya kuombea kv Hisabati, Lugha nk. Hakuna malipo yoyote. Mathayo 10:8 “Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.”

Baada ya maombezi haya hatutawalaumu watoto kwa kila kitu. Tangu nianze maombezi haya wiki hii kwa watoto wangu nimegundua kwamba changamoto zao zingine zilipandikizwa na adui na hazisababishwi na wao wenyewe.

Piga simu hizi kwa ajili ya maelekezo: 0775-591345; 0657-528477; 0712-924234

Dr Lawi Mshana

Post a Comment

0 Comments