Ticker

6/recent/ticker-posts

SIKU 5 MBINGUNI NA KUZIMU (SAFARI YA KWANZA)

Siku 5 Mbinguni na Kuzimu (Safari ya kwanza) 
Bernada Fernandez 

Jiandae kwa kurudi kwa Bwana Yesu! Siku 5 Mbinguni na Kuzimu Habari unayokwenda kuisoma, ni sehemu ya kwanza ya ushuhuda wa dada Bernarda Fernandez, ambaye alipata bahati ya kuchukuliwa na Bwana Yesu Kristo kutembelea ulimwengu ujao. 

HUU NI USHUHUDA WA SAFARI YANGU YA KWANZA 

Kwa kuwa nilikuwa sijisikii vizuri asubuhi hiyo, mume wangu aliona si vizuri aende kazini na kuniacha mwenyewe. Hata hivyo nilimwambia kwamba siko mwenyewe. Baada ya kuondoka tu, nilijisikia kama nakufa. Hivyo niliamua kuwapigia simu baadhi ya marafiki zangu, na mama mkwe. Mama mkwe alinijibu: "Bernarda, Mungu atakubariki leo, usiogope". Jibu lingine linalofanana na hilo lilikuja kutoka kaka mwingine mpendwa katika Bwana, ambaye nilimpigia, lakini aliongeza: "Bernarda amka kutoka kitandani mwako na umtukuze Bwana, mlilie na kumhimidi Yeye". Kwa hiyo, licha ya kukosa nguvu nilimlilia Bwana na kusema: “Bwana wewe ndiwe nguvu yangu, njoo unisaidie”. Nilijaribu kusimama, lakini sikuweza kabisa. Sauti yangu haikuweza tena kusikika lakini ndani ya nafsi yangu nilikuwa namlilia Bwana anisaidie kwakuwa nilikuwa nakufa. Ghafla chumba changu kilimulikwa na mwanga mkali kama moto. Mara moja hofu ikatoweka na niliona malaika wakishuka na kutembea ndani ya chumba changu. Niliweza kuwasikia kwa wazi kabisa wakizungumza wenyewe kwa wenyewe, na mara kiumbe wa ajabu akatokea, wa ajabu kuliko malaika. Alikuwa amevaa vazi Jeupe na mkanda wa dhahabu kiunoni. Kifuani mwake kulikuwa na maandishi ya dhahabu yaliyoandikwa: "MWAMINIFU NA WA KWELI". Uso wake ulionyesha upole na upendo. Yesu Kristo alikuwa mbele yangu, Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana. Jina lake libarikiwe! Yesu alinikaribia, akanigusa kichwani na kuniambia : "Mimi ni Yesu niliyekufa kwa ajili yako. Angalia alama hizi mikononi mwangu, bado zipo kwa ajili yako. Nimeshuka chini kutoka katika kiti changu cha enzi kuongea nawe; kuna mambo mengi katika maisha yako unayotakiwa kuyaweka vizuri. Umvivu na unakasirika haraka. Zaidi ya yote, sitaki mkristo wa asilimia 25 wala wa asilimia 95 bali asilimia 100. Kama unataka kufika mbinguni, ni lazima uwe mtakatifu kama Mimi nilivyo mtakatifu; Nimekuja kukuchukua kwa safari". Nilimuuliza: "Bwana ni safari ya kimisheni?" Alinijibu "Hapana". Kisha alishika mikono yangu na kuninyanyua juu, na kuongea nami kwa upendo. Alinipeleka mbali juu mawinguni. Tukiwa juu aliliangalia jiji la New-York Marekani na nikaona uso wake ukiwa na huzuni. Alilia na kusema: "Neno langu linahubiriwa sana, lakini watu hawataki kusikiliza. Dhambi ya jiji hili imefika juu kwa Baba yangu". Jiji limejaa mashoga; miongoni mwao ni Wanasiasa. Bwana akaniambia: "Hii ni Sodoma nyingine, lakini niko hai na hukumu kutoka kwa Baba yangu italishukia jiji hili hivi karibuni". Kisha nilipiga magoti mbele yake wakati nikilia, akaniambia: "Usiogope.Wakati hukumu ikiushukia ulimwengu huu, Kanisa langu halitakuwa duniani". 

Kisha alinirudisha tena kitandani kwangu na kuniambia nimpigie kaka mmoja mpendwa kanisani kwetu. Alinipa jina la kaka huyo. Aliniomba nimjulishe kuwa roho yangu itatoka ndani ya mwili wangu, na hivyo wasiupeleke mwili hospitali wala kuuzika. Badala yake, amwambie mume wangu amwamini Yeye ambaye ndiye Ufufuo na Uzima (Yohana 11: 25). Bwana akaniambia tena: "Mimi ambaye natoa uzima, nachukua roho yako lakini utarudi na kuwaeleza watu waniamini kwa mioyo yao yote. Ye yote aniaminiye hatakufa milele" (Yohana 11:26). Alinyosha mikono yake na niliona mwili mwingine ukitoka ndani yangu. Nilikuwa nimevaa nguo nyeupe na nilikuwa nang’aa kama Bwana anavyong’aa, "Akaniambia angalia! Huu ni mwili ambao wakristo (waliookoka) wote wanaolitii neno langu watakuwa nao muda mfupi ujao". Nilitambua kwamba ninaweza kutoka kupitia katika kuta. Bwana ambaye alikuwa amenishika mkono alisema: "Angalia"! Nilipogeuka, niliona mwili wangu usiokuwa na roho. Akanielezea kwamba mwili wangu wa nyama hauna thamani, bali ni mavumbi tu, na unapokufa unarudia tena kuwa mavumbi kama mwili mwingine wowote wa nyama. Aliongezea kusema kwamba mwili huu mpya nilionao ni mwili wa utukufu ambao ni roho aliyompa mwanadamu. Nilifikiri angeliniongoza moja kwa moja mbinguni, lakini haikuwa hivyo. Tulishuka kupitia kwenye handaki chini ya dunia, na tulipokaribia mahali fulani nilianza kusikia harufu mbaya isiyoweza kuvumilika. Nikasema: "Bwana sitaki kwenda mahali hapo". Lakini tuliingia ndani; mahali pale ni giza zito na hapafai kabisa kuishi mtu. Nilisikia watu wakiteseka, wakilia vilio vya kutisha. Tulipofika mwisho wa lile shimo, tulikaa kwenye mwamba na Bwana akaniambia: "Angalia "! Niliona watu wakiteseka. Kuzimu, watu hutumia muda wao kulia, lakini kila mmoja hulia kivyake hakuna mtu anayemjali mwenzake. Ndugu wapendwa, ndio tu nilikuja kutambua kwamba KUZIMU KWELI IPO. Nililia na kulia, na nilipo mwangalia Bwana, aliniambia: "Zingatia yote uliyoyaona, wala usiyasahau". Nikuwa naangalia kuzimu, watu walikuwa wakikoroma "Uwi! Uwi! Ni milele na milele! Maumivu na chuki milele na milele." Nilimgeukia Bwana na kumuuliza: "Hivi kuna ndugu yangu ye yote aliyeoko hapa kuzimu?" Alinijibu "Sitakuruhusu kuona mwanafamilia yenu". Nilimuuliza tena: "Bwana kuna mtu yeyote ninayemfahamu hapa?" "Ndio", alisema Bwana na “nitakuruhusu kumuona huyo mwanaume”. Ghafla nilimuona kijana anakuja kutoka ndani ya kilindi cha kuzimu: Alikuwa Alexander. Nilimjua kijana huyu kwenye mkutano wa injili ambao mimi na mume wangu tulihudhuria katika Jamhuri ya Dominica. Wakati tulipokuwa katika mkutano huo, nilisikia sauti iliyosema nami, "Amka, ukutane na Alexander ambaye anapita karibu na mahali ulipo. Mwambie asikatae ujumbe unaohubiriwa hapa, kwakuwa hii ni nafasi yake ya mwisho ninayompa". Hii sauti ilikuwa sauti ya Bwana ingawa sikumuona. Nilimwambia Alexander kile alichoniambia Bwana nimwambie. Hivi ndivyo alivyonijibu: "Ninyi watu Mliookoka wote ni wapumbavu. Mnawadanganya watu kwa kuwaambia kuwa Yesu Kristo anakuja, mimi Alexander siamini hilo kuwa ni kweli". Nilimwambia: "Alexander, Mungu anatoa uzima na anauondoa pia uzima wakati wowote atakapo; Alexander, utakufa muda mfupi ujao”. Alinijibu: "Mimi ni kijana sana siwezi kufa, bado nina miaka mingi ya kufurahia dunia hii." Nafasi hii ilikuwa nzuri hasa na ya mwisho kwa Alexander. Mpendwa msomaji, unajua nini kuhusu wewe mwenyewe? Baada ya wiki tatu, Alexander alikufa wakati akiwa mlevi. Mwisho wake ni hapa mahali pa mateso ambapo nilimwona (kuzimu). Biblia inasema wazi wazi kuwa mlevi hatarithi ufalme wa Mbinguni (Galatia 5: 21). Wakati naangalia watu kuzimu, nilimwona Alexander akishambuliwa na minyoo miwili mikubwa. Alikuwa anapiga kelele "Uwi! Uwi! Uwi!" Alikuwa anateswa. Mara aliponiona alinitambua na akaniambia: "Nilichezea nafasi yangu ya mwishwo. Niko hapa leo nateseka. Tafadhali utakaporudi duniani, nenda nyumbani kwangu uwambie familia yangu wamwamini Yesu Kristo na kulitii neno lake, wasije wakaja mahali hapa pa mateso." 

Kisha Bwana alinionyesha maelfu ya watu waliokuwa wakiteseka kuzimu, akaniambia: "Unaona, baadhi yao walikuwa wameokoka walipokuwa duniani. Bado kuna watu wengi duniani wanaotembea mitaani bila kujua wanakwenda wapi baada ya kufa. Tambua kuwa njia ya kwenda mbinguni ni nyembamba sana, na itaendelea kuwa nyembamba zaidi. Kutakuwa na mambo magumu sana duniani, kiasi kwamba utakapopitishwa katika mambo hayo utakuwa safi kama dhahabu, lakini usiogope kwakuwa nitakutangulia kama jemedari Mkuu". Nilimuuliza: "JE KUNA WALIOKUWA WAMEOKOKA HAPA KUZIMU?", Alinijibu: "Ndio, unajua ni kwa nini? Waliniamini lakini hawakuishi sawa sawa na neno langu. Wako wengi, waliokuwa wakionyesha tabia nzuri tu wakiwa kanisani, mbele ya wachungaji wao na familia zao. Lakini walikuwa wakijidanganya wenyewe. Macho ya Baba yangu yanaona kila kitu na anafahamu kila neno, popote pale ulipo. Waambie watu wangu kwamba ni wakati sasa wa kuishi maisha matakatifu mbele ya Baba yangu, mbele ya shetani na mbele ya ulimwengu. Acha shetani asiwe na haki ya kuwanyoshea kidole watu wangu; na dunia pia isiwe na haki ya kuwanyoshea kidole watu wangu. Ni wakati sasa wa kuutafuta utakatifu na kujitoa sadaka "(1 Petro 1: 14-16) Kisha tulienda mahali ambapo ziwa la moto lipo. Tulipokuwa tunakaribia ziwa la moto, nilisikia harufu mbaya sana na Bwana akaniambia: "Kile unachokiona pale ni ziwa la moto, ambalo liko tayari kwa shetani, nabii wa uongo na mpinga Kristo. Sikuandaa mahali hapo kwa ajili ya wanadamu, lakini wale wote ambao hawaniamini kama Mwokozi wao na wale wote ambao hawaishi sawasawa na Neno langu wataingia mahali hapo. (Ufunuo20:14)" Wakati huo nikamwona Yesu analia na akaniambia tena: "Watu wanaoenda kuzimu ni wengi mno kuliko wanaokwenda mbinguni". Kisha Yesu akanionyesha idadi ya watu waliokuwa wanaokufa katika kila dakika na kuniambia: "Angalia! Ni wangapi wanaopotea! Kanisa langu linalala usingizi ukizingatia kuwa limepokea nguvu zangu; Lina neno langu na Roho Mtakatifu, lakini linalala usingizi. Duniani kuna watu wanaohubiri kwamba kuzimu haipo. Nenda kawaambie kwamba hakika kuzimu ipo". Nilikuwa mbali sana na kuzimu lakini niliweza kusikia joto kali. Baada ya hayo tuliondoka kuzimu na kuelekea mbinguni. Tuliendelea kwenda na kufika mbingu ya pili. Katika mbingu hii Bwana alinionyesha jua na nyota na kuniambia: "Angalia nyota hizi, naziita kila moja kwa jina lake. Unaona hili jua, ni nguvu yangu ambayo inawaangazia wote, waovu na wema. Lakini utakuja wakati ambao juu halitaangaza tena, kila kitu kitakuwa giza". 

Tulienda mbali zaidi na kufika mbingu ambayo Mungu anaishi. Pale kuna nyumba nzuri sana. Kuta za nyumba hizi zilikuwa ndefu sana, za dhahabu safi na mawe ya thamani. Kulikuwa na malango kumi na mbili ya lulu, na malaika kumi na mbili katika malango haya. Nilikuwa nafikiri sitaweza kuingia ndani, lakini Bwana aliniangalia na kusema: "Unataka kuingia ndani?" "Oh ndio Bwana! Kweli nataka kuingia." "Sawa ingia ndani, mimi ndimi mlango" (Yohana10:9). Wakati huu niliingia kupitia lango la thamani na nikaona bustani yenye maua mazuri ajabu. "Je unataka kwenda kwenye bustani? Sawa nenda kwani nimeandaa bustani hii kwa ajili yako na watu wangu kwa ujumla". Nilipoingia katika bustani, nilianza kuchuma baadhi ya maua na kuyapanga katika mafungu. Nilikuwa nakimbia kimbia ndani ya bustani kama msichana mdogo. Maua haya niliyoyachuma yalikuwa na rangi mbalimbali na harufu nzuri sana. Baada ya hapo, Bwana alimuita mmoja. Alikuwa ni malaika, mkakamavu na mzuri sana kiasi ambacho siwezi kumuelezea. Bwana akaniambia: "Unamuona huyu, huyu ni malaika Mkuu Mikaeli, ndiye anayeongoza jeshi langu. Angalia tena!" Niliona jeshi kubwa likiwa juu ya farasi na Bwana akaniambia: "Hili sio jeshi la kibinadamu, bali ni jeshi la Baba yangu. Jeshi hili liko tayari kwa ajili ya Wakristo wale ambao KWELI wamezaliwa mara ya pili (Waliookoka); usiogope, kwakuwa jeshi hili lina nguvu kuliko lile lililoko duniani". Kisha akanionyesha malaika mwingine. "Huyu ni mhudumu wa watu Waliookoka wale wanaotii neno langu". Nilifurahi nilipoambiwa hilo: "Uwe makini! Mimi ni Mungu wa Abraham, Mungu wa Musa, Mungu wa Eliya, Yeye aliyesababisha moto kushuka kutoka mbinguni; Sijabadilika. Nakwenda kukuonyesha hali ya watu wangu jinsi wanavyoishi nyakati hizi za mwisho walizobakiza". Bwana akaniambia: "Uwe mwangalifu kwa yale ninayokwenda kukuonyesha ". Nikawaona watu Waliookoka ambao ni dhaifu na waliochoka. Bwana akaniuliza swali hili: "Unaamini kwamba naweza kuchukua Kanisa katika hali yake hii?" Kisha akaniambia, "Wakristo nitakaowachukua ni wale waliojaa utukufu, washindi, wasio na kunyanzi lolote, wasio na hatia yo yote. Miongoni mwa watu wangu wapo waongo, wasio na upendo, watu wangu wamegawanyika. Nimekuonyesha hali ya watu Waliookoka katika siku hizi za mwisho; 

Sasa nakwenda kukuonyesha jinsi Kanisa la kwanza walivyoishi. Wote walijaa utukufu wa Mungu .Walikuwa watu wa maombi ya kufunga mara kwa mara; walihubiri neno langu bila hofu yo yote. Wakati Wakristo (watu waliookoka) wa sasa wanafikiri kuwa nimebadilika, na pia wanafikiri Roho Mtakatifu amebadilika. Kosa kubwa la watu waliookoka wa sasa ni kuishi maisha ya mazoea yaliyoandaliwa na mwanadamu. Kwahiyo wamesahau kuwa jumbe zinatoka kwa Roho Mtakatifu na mbinguni. Waambie watumishi wangu, wachungaji kwamba wakati umefika kuachana na program (vipindi) za mazoea. Wakiziacha, wataziona nguvu za Mungu katikati yao, Roho Mtakatifu aliyejidhihirisha katika Kanisa la kwanza, Atafanya miujiza, ishara na maajabu makubwa hata wafu kufufuliwa. Roho Mtakatifu ni Yule Yule, ni ninyi tu mliobadilika ". Wakristo mliookoka ni wakati wa kurudi katika maisha ya Kanisa la kwanza. Kisha nikaondoka katika bustani hii nzuri na kwenda katika barabara za dhahabu na Bwana akaniambia: "Gusa! Ndio ni dhahabu safi. Nenda kawaambie watoto wangu kwamba MUDA MFUPI SANA UJAO, wanakwenda kutembea katika barabara hizi za dhahabu kwa mkono wa Yule anayetoa uzima (Ufunuo wa Yohana 21:10-15)" Oh! Ni furaha ya kiasi gani kutembea katika barabara hizo za dhahabu! Baada ya hapo niliona Kiti cha enzi kilichojaa utukufu kilichozungukwa na Malaika, Malaika wakuu na Maserafi. Walikuwa wakiendelea kumsifu Mungu Yule aliyekaa katika kiti cha enzi, wakisema: "Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ni Bwana Mungu Mkuu; mbingu na nchi zimejawa na utukufu wa Mungu. Amen!" Wakati umefika wa kuinua mikono iliyo safi kwangu na kunitukuza alisema Bwana Yesu". Wakati huu huu nikaona mto wa maji ya uzima ukipita katikati ya kiti cha Enzi. Niliona pia mti wa uzima na kwa upande mwingine niliona upinde wa mvua na mto wa kioo. Kisha, nikamuuliza Bwana: "Ni nani aliyekaa katika kiti cha Enzi?" Akanijibu: "Ni Baba yangu, Bwana wa Majeshi". Nikamwambia : "Naweza kumwona Baba", "Hapana muda haujafika", Bwana alinijibu. Hata hivyo ingawa sikumuona Baba uso wake, Yule aliyekuwa katika kiti cha enzi alikuwa Mkuu sana. Niliona ngurumo na miali ya mwanga ikitoka katika kile kiti cha enzi na nilisikia sifa. Yesu aliniambia: "Unasikia sifa hizi? Hizi ni sifa zinazoimbwa na wale waliokombolewa". Niliwaona malaika saba, kila mmoja alishika kitasa cha dhahabu; na malaika wengine saba kila mmoja alishika tarumbeta. "Bwana hawa malaika wanafanyaje?" Bwana akanijibu: "Hivyo vitasa saba vilivyoshikwa na malaika zimejazwa ghadhabu ya Mungu. Muda mfupi ujao vitamiminwa na tarumbeta zitakapopigwa, Kanisa langu (wale wanaoishi sawa sawa na mapenzi ya Baba yangu) watanyakuliwa. Hawatakuwa tena duniani wakati wa dhiki kuu. Kabla ya mpinga Kristo hajajidhihirisha, Yule mtu wa kuasi, Kanisa langu watasikia tarumbeta ya mwisho ikipigwa, na watakutana nami hewani (1 Thesalonike 4:16). Rafiki mpendwa nilipokuwa pale, mbele ya kiti cha enzi, sikuwa na habari na muda. 

Muda mfupi baadaye Yesu akanionyesha jinsi Kanisa lake (waamini wa kweli) litakavyo nyakuliwa. Niliona katika maono, maelfu ya watu wakitoweka duniani. Hii ilitokea kwa ulimwengu mzima, TV na redio zinatoa habari za kutoweka huku kwa watu. Magazeti yakiwa na vichwa vya habari vyenye rangi nyekundu nayo yalitoa habari hizi. Bwana akaniambia: "Habari hizi zitatokea muda mfupi tu ujao". Hukumu ya Baba yangu haijaja duniani, kwa sababu ya watu Waliookoka waaminifu, ambao kweli wananipenda." Baada ya hayo, niliona yule mtu wa kuasi. Alikuwa anawaambia watu wakaao duniani: "Ninawaletea amani na usalama" na mara watu wakasahau kile kilichotokea muda mchache uliopita (unyakuo wa Kanisa). Bwana Yesu akaniambia: "Angalia kwa makini!". Nikaona katika maono malaika saba wakiwa na vitasa saba. Ndugu mpendwa, kile kilichokuwa kikitokea ni vigumu hata kusimulia; Niliona malaika saba wakimimina vile vitasa saba vya ghadhabu ya Mungu duniani. Tarumbeta zilianza kulia. Mungu alikuwa anamimina ghadhabu yake kwa wote wakao duniani, na nchi zote zikatoweka. Bwana akaniambia: "Angalia! Watu hawa ambao walikuwa ni sehemu ya Kanisa langu (walikuwa wameokoka), wengine walikuwa ni wachungaji ". Kwa kuwa sikulielewa hili vizuri nilimuuliza Bwana: "Inakuwaje watu wako wengi hivi wameachwa na kuingia katika dhiki kuu? Hii inakuwaje hata kuna wachungaji katikati yao ambao walihubiri neno lako?" Bwana Yesu alinijibu: "Ndio, walihubiri neno langu, lakini walikuwa hawaishi sawasawa na neno langu." 

Kisha Bwana akaniruhusu nione umati mwingine wa wachungaji, na akaniambia: "Wachungaji hawa walikuwa hawahubiri neno langu kama lilivyoandikwa. Walifikiri kuwa neno langu haliendani na karne hii. Walikuwa wanawapendelea wale wanaotoa fungu la kumi kubwa, kwasababu walikuwa wanapenda vitu vya duniani. Nenda uwaambia watumishi wangu Mimi ndiye niliyewaita, na kwamba fedha na dhahabu ni mali yangu na ninawapa kutokana na ukuu na utukufu wangu. Waambie wahubiri neno langu kama lilivyoandikwa. Wako wengi ambao wanatoa tafsiri isiyo sahihi ya neno langu. Neno langu ni neno langu, hakuna mtu ye yote anayeweza kulibadilisha. Ni lazima lihubiriwe kama lilivyoandikwa. Kuna wengi miongoni mwa watu wangu wanaolipotosha neno langu kwa ajili ya maslahi yao wenyewe ". 

Baada ya hayo, tuliingia kwenye verenda katika mji mpya wa Yerusalem na Bwana akaniambia: "Unachokiona ni paradiso". Pale Paradiso niliwaona mitume na nikamuuliza Bwana, Bwana Ibrahimu yuko wapi? Nilikuwa nategemea kumwona mzee, lakini ghafla nikaona kijana wa umri wa miaka 25 hivi anakuja na Yesu akaniambia, huyu ni Ibrahimu baba wa Imani. Bwana alimwita mwanamke mzuri sana mwenye uzuri usioelezeka, kama wengine wote niliowaona pale, na akaniambia: "Huyu ni Maria ! Nenda ukamwambia kila mmoja kwamba Maria sio Malikia wa mbinguni. Mfalme wa mbinguni ni Mimi, mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana; Yeye asemaye: "MIMI NDIMI NJIA, KWELI NA UZIMA . (Yohana 14: 6-7). Nenda ukakiambie KIZAZI hiki KILICHOPOFUSHWA MACHO kwamba hakuna pulgatori, kama ingelikuwepo ningekuonyesha. Badala yake, kuna kuzimu, ziwa la moto na mji Mtakatifu wa Yerusalem, na paradiso ambayo nimekuonyesha. Lakini waambie kwamba hakuna pulgatori; waambie kwamba huo ni UONGO WA IBILISI, HAKUNA PULGATORI ". 

Kisha Bwana aliniongoza kwenye stoo ya kuhifadhia taji. "Hizi ni taji za uzima, alisema Bwana Yesu". Baadaye Bwana akaniuliza tena : "Unaona nini?" Ninaona Kanisa langu ninakoabudia kule duniani, washirika wa kanisa hili, wanaimba na kuhubiri lakini majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima, hivyo nikamuuliza Bwana Yesu: "Kwanini majina ya washirika wa kanisa langu hayajaandikwa katika kitabu hiki?" Akaniambia: "Kwasababu ya maovu yao wanayotenda duniani". Baada ya haya yote Bwana akaniruhusu kurudi duniani.


Post a Comment

0 Comments