Ticker

6/recent/ticker-posts

NINI MAANA YA KUIBIWA NYOTA KWA MUUMINI WA KWELI (SEHEMU YA PILI)


NINI MAANA YA KUIBIWA NYOTA KWA MUUMINI WA KWELI (Sehemu ya pili) 

Katika somo lililopita (sehemu ya kwanza) nimetoa maandiko kadhaa kuhusu nyota kwa mtazamo wa ki-Biblia. 

Shetani anaiba nini katika maisha ya watu? Yn 10:10 “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.” 

1. Kusudi (Purpose): Kusudi ndilo linaleta tafisiri na maana ya maisha. Maisha yasiyo na kusudi hayana maana. 

2. Shauku (Desire): Shauku ya moyo ikifa, kuchanganyikiwa kunaingia. Ukiibiwa shauku hutakuwa na moyo wa kufanya unachokifanya. 

3. Maono (Vision): Maono yanakupa hatua nyingine. Maono yakifa, kudumaa kunatawala. 

4. Karama (gifts): Karama inafungua mlango wa kusikilizwa. Hutakuwa mtu muhimu kama karama imezikwa. 

5. Matunda ya mwili wako (The fruit of your body): Shetani anapenda kuharibu kizazi chako yaani, watoto na wajukuu zako. 

6. Matunda ya kazi zako (The fruit of your labour): Furaha ya shetani ni wewe ufanye kazi kwa bidii lakini usiwe na kitu cha kuonyesha (faida). 

7. Ndoa yako (Your Marriage): Ndoa zinavunjika kila kukicha. Ndoa zikiwa na mgogoro, kanisa na taifa litayumba. 

8. Wito wako (Your Calling): Shetani hataki utimize huduma yako. Ukitimiza huduma maana yake umeushinda ufalme wa shetani. 

9. Uwezo uliojificha (Your Potential): ‘Potential’ ni kile unachoweza lakini hujakifanya. Usipojua uwezo wako utakuwa na maisha yasiyo na utoshelevu. 

10. Sauti yako (Your voice): Kila mtu amepewa sauti na Mungu. Shetani anafurahi akinyamazisha sauti yako na kupoteza mamlaka yako. 

11. Mafanikio ya kazi yako (Your career): Shetani akishambulia unachoweza kufanya, unakuwa na mapambano yasiyoisha. 

12. Jina lako (Your name): Shetani pia anafuta majina ambayo ni tishio kwa ufalme wake wa giza. Unaweza kujikuta unapachikwa jina lenye maana mbaya ili usifanikiwe. 

13. Misheni au hatima yako (Your destiny): Misheni yako ikiuawa, unakuwa maiti inayotembea. 

14. Ahadi za Mungu (The promises of God): Shetani akishambulia ahadi za Mungu kwako, hazitatimia. Utakuwa siku zote kwenye BONDE la ahadi badala ya KILELE cha ahadi. 

15. Maisha yako sasa na baadaye (Your present and future life): Shetani hataki mtu yeyote atimize siku zake hapa duniani. Pia hataki mtu yeyote aende mbinguni. 

Ushuhuda hai: Mmiliki mmoja wa Clinic ambapo wanawake wanajifungulia, alipookoka aliuliza mtumishi kama Mungu anasamehe kila dhambi. Akaambiwa mtu akitubu kwa kumaanisha anasamehewa dhambi ya aina yoyote. Mmiliki huyo akasema alikuwa anakusanya nyota za watoto wanaozaliwa na kuziuza. Siku moja aliona mtoto ambaye nyota yake ya 7 ni ya utajiri akaichukua. Akaendelea kusema, ‘Huyo kijana hata sasa baada ya mimi kuokoka namfahamu. Kijana huyo kwa sasa anabeba mizigo sokoni wakati alipaswa kuwa tajiri mkubwa.’ 

Dr Lawi Mshana, +2557129242434; Korogwe, Tanga, Tanzania

Post a Comment

0 Comments