Ticker

6/recent/ticker-posts

MAISHA YAKO NI MAGUMU KWA VILE UMEIBIWA AU KUBADILISHIWA NYOTA YAKO


MAISHA YAKO NI MAGUMU KWA VILE UMEIBIWA AU KUBADILISHIWA NYOTA YAKO

Shetani anaweza kukuibia hatima yako na kujikuta ukiishi maisha ambayo hukupangiwa na Mungu. Yn 10:10 “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.” Bwana Yesu alipozaliwa wapo walioiona nyota yake ya Ufalme ingawa hawakuwa na nia mbaya. Mt 2:1,2 “Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.” Shetani mwenyewe alikuwa na utukufu (alikuwa nyota ya alfajiri). Isaya 14:12 “Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!” Shetani anajua sana kuhusu nyota. Ingawa hawezi kuiharibu nyota yako, anaweza kuihamishia kwa mtu mwingine. 

NB: Zipo dalili nyingi (hata hivyo sio wakati wote zinahusiana na kuibiwa nyota yako). 

Ngoja nikutajie baadhi ya dalili za kuibiwa nyota yako na wachawi: 

1. Watu kujenga chuki na wewe bila sababu za msingi. 
2. Unafanya kazi kwa bidii sana lakini hupati faida (hata ufanye kazi kwa bidii vipi hakuna maendeleo). 
3. Unakuwa na maisha yasiyobadilika hata kama unapata pesa (udumavu wa maisha). 
4. Unakuwa masikini kiasi kwamba masikini wengine wanakuita masikini. 
5. Ugumu wa kuoa/kuolewa au kudumu katika ndoa unaojirudia. 
6. Kutawaliwa na magonjwa mengi yasiyosikia dawa wala kuonekana katika vipimo vya maabara. 
7. Kufanya kazi muda mrefu bila kupandishwa daraja au cheo hata kama sifa unazo (wakati waliokukuta wenye sifa kama zako wanapandishwa). Nk 

Hata hivyo kuibiwa nyota kunatokana na uhusiano uliowahi kuwa nao na watu fulani (wewe mwenyewe au wazazi wako) na ndoto unazoota zilizopandikizwa na wachawi. Hizo ni baadhi tu ya dalili. 

Dkt. Lawi Mshana, +255712924234; Korogwe, Tanga, Tanzania

Post a Comment

0 Comments